25 November 2013

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inasheherekea maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake huku yakiwemo mafanikio makubwa dhahiri na ya kujivunia katika sekta ya mawasiliano nchini.
TCRA ilianzishwa rasmi mnamo tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2013 ili kusimamia Sekta ya Posta na Mawasiliano ya Elektroniki ikkiwemo simu, utangazaji, wavuti pamoja na huduma za Posta. TCRA ilkianzishwa kwa Sheria Na. 12 ya mwaka 2003 iliyoziunganisha Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).
Mkakati mahususi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ni “Kuboresha Maisha ya Watanzania kupitia mfumo makini na thabiti ili kuhakikisha kunakuwa na huduma za mawasiliano kwa wote nchini”.   Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, Tanzania imeshuhudia kukua kwa kasi kwa Sekta ya Mawasiliano. Mamlaka ilianzisha mfumo wa leseni za Muingiliano mnamo tarehe 23 Februari 2005.

Mfumo huu wa leseni za muingiliano (Convergence Lisensing Framework) umekuwa chachu ya kuongezeka kwa miundombinu mbalimbali ya mawasiliano, huduma mbalimbali kwa kutumia mtandao wa mawasiliano ikiwemo wavuti (internet) na utangazaji.
Makampuni ya simu yameongezeka kutoka kampuni moja ya simu TCRA ilivyoanzishwa mwaka 2003 hadi kufikia makampuni saba (7) yenye wateja wenye laini za simu takribani milioni 28 kulinganisha na idadi iliyokuwepo miaka kumi iliyopita. Huduma za simu za mkononi zimebadilisha maisha ya Watanzania kutokana na huduma mbalimbali zinazopatikana kupitia simu za mkononi. Kuanzia huduma za kutuma fedha kupitia simu, malipo ya Ankara mbalimbali na huduma nyingine nyingi zilizobadilisha maisha na uchumi wa wananchi wa taifa hili.
Sekta ndogo ya Posta nayo haijabaki nyuma kwani kumekuwepo na ongezeko la watoa huduma kutoka mmoja hadi zaidi ya hamsini wenye kutoa hduma ndani nan je ya Tanzania. Tunatarajia mabadilikjo makubwa kwa watanzania hasa baada yan kukamilika kwa mradi wa anwani mpya za makazi na misimbo ya Posta.
Hali kadhalika, yako mabadiliko makubwa sana katika msekta ndogo ya utangazaji. Kutoka nchi yetu kuwa na Radio moja hadi Zaidi ya redio 85. Aidha kutokuwepo kwa Kituo cha Utangazaji wa Runinga hadi vituo vya utangazaji vipatavyo 26. Watumiaji wa wavuti (intanet wameongezeka kutoka watumiaji million moja hadi takribani milioni 8 na ushee. Sekta ya Mawasiliano imekuwa chimbuko la maendeleo ya nchi kwa kutoa ajira kwa watanzania wengi na hali kadhalika kuongeza mapata ya serekali kwa tozo na kodi mbalimbali zinazotolewa katika sekta..
Mamlaka ya Mawasiliano imeshinda tuzo mbalimbali katika masuala ya Udhibiti na Usimamizi Bora wa Huduma za mawasiliano nchini katika kipindi cha kuweko kwake miaka kumi iliyopita. Nchi mbalimbali zimekuja Tanzania kujifunza udhibiti na usumamizi wa masuala nyeti ya mawasiliano kama vile masuala ya uhamaji kuelekea mfumo mpya wa utangazaji wa dijitali, Mifumo ya uanzishwaji wa anwani  za makazi na misimbo ya posta, Usimamizi mzuri wa masafa na namba za mawasiliano na mambo mengine mengi.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MAADHIMISHO TANGU 25 – 29 NOVEMBER 2013
Katika kusheherekea miaka kumi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, kutakuwa na maadhimisho ya wiki nzima yenye matukio mbalimbali. Tukianzia na mkutano huu na waandishi wa habari uliokusudia kutoa taarifa kwenu na kwa wananchi kuhusu maadhimisho haya, kutakuwa na matukio kadha wa kadha kuelekea kilele cha sherehe za maadhimisho yanayotarajiwa kufanyika tarehe 29 Novemba 2013.Maadhimisho haya yanafanika chini ya kauli mbiu ya; Miaka 10 ya TCRA: Miaka Kumi ya Mapinduzi Katika Sekta ya Mawasiliano
Kesho tarehe 26 Novemba 2013 kutakuwa na tukio maalumu kwa wafanyakazi wa mamlaka ambapo wale waliokuwepo tangu wakati wa kuanzishwa kwa TCRA watatunukiwa vyeti pamoja na zawadi mbalimbali kutambua mchango wao kwa taasisi.
Aidha siku ya tarehe 27 Novemba 2013; kutakua na sherehe ya kutoa udhamini kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya elimu ya juu wanaochukua masomo ya mawasiliano, sayansi na teknolojia. TCRA kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo imekuwa ikitoa udhaminim katika masomo hayo kwa wanafunzi mahiri kwa nia ya kukuza weledi na kuboresha utumishi katika sekta ya mawasiliano chini ya kinachoitwa “TCRA ICT SCHOLARSHIPS” kwa wanafunzi wa digrii ya kwanza, digrii za Uzamili na Uzamivu.
Kuanzia tarehe 27 – 29 Novemba, kutakuwa na maonesho maalumu katika viwanja vya ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ambapo watoa huduma mbalimbali za mawasiliano nchini wataonesha mafanikio yao na huduma wanazotoa kwa wananchi. Napenda kuchukua fursa hii kuwasihi waandishi wa habari kuhudhuria maonesho haya ili kujifunza na kutumia fursa hiyo kuelimisha jamii ya watanzania kuhusu huduma mbalimbali za mawasiliano zinazopatikana nchini ili wachangamkie fursa.
Hali kadhalika, katika maadhimisho haya, TCRA imeandaa washa maalumu ya siku mbili wa wadau wa mawasiliano kujadili fursa, changamoto pamoja na namna gani kwa pamoja tunavyoweza kufanya mawasiliano kuwa bora Zaidi nchini mwetu. Warsha hiyo itafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na itafunguliwa rasmi tarehe 28 mwezi huu na Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utaendelea hadi tarehe 29 Novemba 2013.  The Opening Ceremony will be graced by Dk. Mohammed Gharib Billal.
Wadau mbalimbali wa Mawasiliano kama vile kituo cha Habari cha Tanzania Network Information Centre (tzNIC), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote - Universal Communications Services Access Fund (UCSAF), Wamiliki wa Vyombo Vya Habari - Media Owners Association of Tanzania (MoAT- Broadcasting), na Umoja wa Makampuni ya Simu - Mobile Operators Association of Tanzania (MoAT-Mobile Telephony Companies), Africa Media Group, Agape Associates and TTCL watawasilisha mada mbalimbali.
Vyombo vya Habari vinakaribishwa katika shughuli zote za maadhimisho ya Miaka 10 ya TCRA ili kutoa elimu kwa umma lakini pia kama fursa ya kujionea mafanikio ya sekta ya mawasiliano katika kipindi cha miaka kumi iliyopita ili kuwawezesha wananchi kufahamu tulikotoka, tunakoenda na fursa zilizoko katika sekta ili kuboresha maisha yao.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!