15 November 2013

Kuelekea siku ya ukimwi duniani,ambayo huadhimishwa tarehe moja mwezi wa kumi na mbili kila mwaka taasisi zisizo za kiserikali za TASUBA,na Umoja wa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Bagamoyo (UWAMABA) na Ushahuri Nasaha na Kupima (UKUNI) wanazikaribisha kurasa,na makundi mbalimbali zilizomo katika mitandao ya kijamii kuungano nao ili kuweza kushiriki katika maadhimisho hayo.

Taasisi hizo zisizo za kiserikali zinakaribisha kurasa,na makundi yote yaliyopo katika mitandao hiyo ya kijamii ili yaweze kushiriki  katika kuungana kwenye tukio muhimu majadiliano,warsha, kupima, kutoa elimu, sahihi juu ya Kupunguza maambukizi mapya ya VVU na Ukimwi.

Akizungumza na Blog ya Tmark mratibu wa warsha hiyo bwana Andrew Chale,alisema warsha hiyo inatarajia kuanza novemba 29 hadi desemba 2 katika chuo cha sanaa kilichopo mjini bagamoyo.

Alisema dhumuni la kushirikisha makundi na kurasa zilizopo katika mitandao ya kijamii,wanaamini kwa kupitia wao watakuwa wameilimisha jamii nzima ya watanzania.

''Tunakaribisha magroup na kurasa mbalimbali za facebook,Instragram,tweeter,whatsup,badoo, nk. katika kuungana kwenye tukio muhimu majadiliano,warsha, kupima,na kutoa elimu sahihi juu ya Kupunguza maambukizi mapya ya VVU na Ukimwi,kwani tunaamini kuwashikisha wao kunaweza kupunguza maambukizi hayo''alisema bwana Chale

Alisema kauli mbiu ya warsha hiyo ni "MITANDAO YA KIJAMII INAWEZA KUSAIDIA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI NA KUONDOA UNYANYAPAA KWA JAMII"...CHUKUA HATUA TUITUMIE KWA ELIMU SAHIHI.

Mratibu huyo alisema ili kuweza kufanikisha warsha hiyo wanahitaji wawezeshaji,wadau  kujitokeza ili kuweza kudhamini.
Alisema kwa yoyote atakae guswa kudhamini warsha hiyo anaweza kuwasiliana nao kwa namba 0719-076376 / 0767076376.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!