6 November 2013

 

Stori: Mwandishi Wetu, Musoma

Msichana mmoja, Mariam Chacha, mkazi wa Mtaa wa Nyasho A, mjini hapa amemwagiwa maji ya moto na kuunguzwa mwili, hali iliyofanywa alazwe katika hospitali ya mkoa.

Mariam Chacha baada ya kumwagiwa maji ya moto.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Oktoba 22 mwaka huu saa mbili usiku ambapo inadaiwa aliyefanya kitendo hicho ni Pendo Wambura ambaye amekamatwa na polisi.
Habari kutoka ndani ya kituo cha polisi mjini hapa zinadai kuwa mara baada ya Mariam kumwagiwa maji ya moto na mwenzake na kuungua sehemu za kitovu mpaka usoni, matiti na mikono na akiwa hajitambui mpaka sasa, wasamaria wema walimpeleka polisi ili kupata hati ya matibabu (PF 3) na akaenda kutibiwa katika Hospitali ya Serikali ya Musoma alikolazwa wodi namba nne.
“Polisi tulikwenda kumkamata mtuhumiwa na tunamshikilia kwa kuwa majeruhi hali yake ni mbaya, kalazwa, na tayari amefunguliwa jalada namba MUS/IR/5009/013,” alisema afisa mmoja wa polisi kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini kwa kuwa siyo msemaji.
Shuhuda mmoja aliliambia gazeti hili kwamba Mariam alikwenda kuwasalimia ndugu zake pamoja na mama yake ambaye ni mgonjwa wanaokaa nyumba moja na mtuhumiwa.
“Mariam alipoona hali ya mama yake alianza kulia ndipo Pendo alipokwenda kuchukua maji yaliyokuwa yakichemka ili yapikiwe ugali wa mama mwenye nyumba na akamwagia mwenzake akidai eti anachukizwa na kitendo chake cha kumlilia mgonjwa wake,” kilisema chanzo.
Global  publisher
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!