31 July 2012


Kanye that dress code suck...mmmh etiii they look horrible  hahahahaha kimmy uwe unamshauri mwenzio kuvaa basi maaana mmmh


Waandishi watamani leseni za fani yao 

BAADHI ya waandishi wa habari mkoani Morogoro, wamependekeza  kuwa Tasnia ya Habari Nchini, ianzishe bodi ya usimamizi wa maadili ya waandishi wa habari, kama katika  taaluma zingine, ili kudhibiti mmomonyoko wa maadili ya fani hiyo.

Hatua hiyo inafuatia kukithiri kwa vitendo vya mmomoyoko wa maadaili katika tasnia hiyo licha ya kuwepo kwa jitihada za kutoa mafunzo na miongozo mingi  inayotolewa na taasisi mbalimbali likiwemo Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Wakizungumza katika semina ya siku tatu ya maadili ya waandishi wa habari mkoani Morogoro , waandishi hao walisema kuna haja ya kuwa na bodi ambayo moja ya ma jukumu yake ni  kutoa leseni kwa waandishi wa habari na kudhibiti mienendo ya  waandishi wa habari.

Mmoja wa washiriki wa semina hiyo, Nikson Mkilanya, ambaye ni mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha  Star na Redio Free Africa, alisema ikiwa waandishi wenye sifa watapatiwa leseni, itakuwa ni rahisi kuwadhibiti wasiokuwa waandishi ambao wamekuwa wakifanyakazi kama wanahabari wengine, pasipo kudhibitiwa.

Mkilanya alisisitiza kuwa hatua hiyo itapunguza wimbi la makanjanja na kuimarisha heshima ya taaluma hiyo.
Mtoa mada katika semina hiyo, Juma Thomas, ambaye ni  mwandishi wa habari na wakili wa kujitegemea, alisema hoja hiyo ni ya msingi na kupendekeza kuwa waandishi wa habari watumie fursa ya kutoa maoni kuhusu katiba mpya, ili sheria iliyopo iboreshwe.

Thomas  alisisitiza kuwa waandishi wa habari wamekuwa katika mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa sheria zinazokandamiza uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kupata na kutoa habari, zinaondolewa na kwa mantiki hiyo lazima wafanye hivyo katika kushughulikia suala la leseni zao.

Alisema wadau wa tasnia ya habari wamekuwa wakihangaika ili kuhakikisha kuwa mswada wa mabaoresho ya sheria kandamizi unafikishwa bungeni lakini imeshindikana kwa sababu zisizofahamika.
Waandishi wengine walipendekeza kuwa MCT inaweza kubeba jukumu la utoaji leseni na kuendelea kusimamia maadili ya waandishi wa habari nchini.

Tume iliyoundwa na nchi zisizofungamana na upande wowote mwaka 1980 kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni ( UNESCO) ilitoa mapendekezo ya kupinga waandishi wa habari kuwa na leseni kama ilivyo kwa tasnia zingine kwa madai kuwa hatua hiyo inakwenda kinyume na haki za binadamu za kupata na kutoa habari.
Mwenyekiti mstaafu wa Moropc, Bonventure Mtalimbo, alisema kuwa zoezi la utoaji wa vitambulisho vya waandishi wa habari (press card) ambalo limekuwa likifanywa na Idara ya Habari Maelezo kama mbadala ya leseni limeonekana kukwama kutokana na utaratibu mbovu uliopo.

Alisema kuwa vitambulisho hivyo vimekuwa vikichelwa kutolewa na ukomo wake wa mwaka mmoja umekuwa ukitafisiriwa kuwa ni aina ya biashara ambayo hufanywa na idara hiyo huku idadi ya wanaovitapa ikizidim kupungua kila mwaka.

Gazeti la mwananchi
Venance George, Morogoro

30 July 2012




Muigizaji wa filamu za kibongo Hemed Suleiman  amesema yeye hana mazoea ya kutumia kinga wakati akifanya mapenzi.

Hemed ameyasema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na mbunifu wa Single buttons kivazi ambacho kimejizolea umaarufu sana Bongo, na mmiliki wa blog ya mvutokwanza Martin Kadinda.

Alisema ameshatembea na mastaa wenzake wa kike wapatao 32 hadi sasa kwa hesabu zake za haraka haraka na kuwa kwa mastaa hao hakuna hata mmoja aliyetumia nae kinga.

Hemedi ambae ameendelea kujitapa kuwa yeye ndio bingwa wa kucheza na mioyo wa mabinti wa kibongo na ndio maana wanamuita hemed PHD.

Ameendelea kuwananga wasichana hao kuwa kutokana na kutovutiwa nao na ndio maana huwa anapita tu,kwa kuwa huwa anakuwa na hamu ya kufanya nao mapenzi kwa wakati huo na hasa asipokuwa na uhusiano wa maana na mtu yoyote kwa wakati huo.

Aliongeza miezi mitatu aliyopita alikuwa katika  mahusiano na msichana mmoja ambaye hajataka kumtaja jina, na sasa wameshaachana  ila aliwahi pima nae virusi vinavyopelekea ugonjwa wa Ukimwi.
zaidi ingia:www.mvutokwanza.com



BAADA ya kutamba kwa muda mrefu katika muziki wa kizazi kipya nchini, msanii nyota wa muziki huo, Naseeb Abdul ‘Diamond’ amesema anafikiria kujitosa katika muziki wa taarab. Diamond alisema Jijini Dar es Salaam wiki hii kuwa,amefikia uamuzi huo kutokana na kuvutiwa na muziki huo wa taarab.
 Mshindi huyo wa tuzo mbalimbali za muziki za Kilimanjaro amesema, anajua uamuzi wake huo utawashangaza mashabiki wengi, lakini ni jambo la kawaida kwa msanii. 
 Diamond alisema hadi sasa anaamini hana mpinzani katika muziki wa kizazi kipya na hakuna msanii anayeweza kufikia kiwango chake hapa nchini.
 Diamond alisema ameamua kupiga miondoko tofauti ya muziki kutokana na kipaji alichonacho katika fani hiyo, ambayo imempatia umaarufu mkubwa, Kutokana na kipaji chake hicho,Diamond alisema hakuna kitu anachoshindwa kukifanya katika fani ya muziki.
 Alisema bado hajaanza rasmi kupiga muziki wa taarab,na kuwa sasa anafanya tathmini ya soko la muziki huo ili kuona kama unaweza kumletea mafanikio kama ilivyo kwa muziki wa bongo fleva. 
 Alisema anaweza kufanya kila aina ya muziki kwa sababu anakipaji cha kuimba nyimbo aina zote, hivyo endapo atafikia muafaka anaweza kufanya muziki wa taarabu. 
 Diamond alikiri kuwa, muziki wa kizazi kipya umemfanya ajulikane sehemu nyingi duniani, ikiwa ni pamoja na kupata manufaa mbalimbali kimaisha kwa kuishi kwenye nyumba nzuri na kumiliki magari ya kifahari.


source:www.jukwaahuru.com 

24 July 2012


WEMA SEPETU ATOA MSAADA KATIKA KITUO CHA WATOTO WA KITUO CHA GOOD HOPE JIJINI ARUSHA

 My gal na mmoja kati ya mtoto anaelelewa katika kituo cha good hope
 Akikabidhi dola elfu moja taslim
Kilio hiki kilikuwa cha furaha,hakika kilio humaanisha mengi jamani.

tmark-turn,tunakutakia kila kheri wema sepetu kwa upendo wako uliouonyesha na usiishie hapa uwasaidie na wengine inshallah,mwenyezimungu akuzidishie upendo na amani,akuondelee mabaya .amina
Picha toka:http://mvutokwanza.blogspot.com/
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ametajwa kuwa kichocheo cha kurejea kwa penzi la vijana wenye umaarufu mkubwa nchini kwa sasa, Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’ na Wema Isaac Sepetu. Uwazi, lina mkanda wa video, unaowaonesha Diamond na Wema pamoja kwa mara ya kwanza, baada ya muda mrefu wa kutupiana maneno mengi ya kashfa, huku kila upande ukimshusha hadhi mwenzake.

SAFARI ILIVYOKUWA TAMU
 Watu wengi wakijua kwamba kuna uhasama mkubwa kati ya Wema na Diamond, Julai 17, mwaka huu, ilikuwa ni mshangao wa aina yake kwa waliokuwepo Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Kigoma, baada ya vijana hao kushuka wakiwa wameongozana. Diamond akiwa amevaa shati jekundu na tai nyeusi, chini akiondokea suruali ya jeans rangi ya bluu iliyopaushwa kimodo, huku Wema akitokelezea kwa koti la rangi ya maziwa, ndani blauzi nyeusi, halafu wote wameyaficha macho yao kwa miwani nyeusi, waliwaka vilivyo ndani ya Ujiji, Kigoma. Baada ya kuwasili Kigoma, Wema na Diamond walielekea Hoteli ya Tanganyika Beach (ipo ufukweni mwa Ziwa Tanganyika) ambako walipata pumziko walilohitaji kabla ya nyota huyo wa wimbo wa Mbagala, hajaelekea Uwanja wa Lake Tanganyika kwenye Tamasha la Kigoma All Stars a.k.a Leka Dutigite

WEMA ALIFUATA NINI KIGOMA? Minong’ono ilitawala kila kona ya Mkoa wa Kigoma kwamba Wema amekwenda kuwakilisha Leka Dutigite, hivyo wakataraji kumuona Uwanja wa Lake Tanganyika, akitoa sapoti yake kwenye tamasha hilo. Wapo ambao waliacha shughuli zao kwa ajili ya kwenda kumuona Wema tu uwanjani lakini waliambulia patupu, kwani mrembo huyo hakuonekana kabisa. Kutokana na hali hiyo, wale waliovumisha stori kwamba Wema amekwenda Kigoma a.k.a Lwama, walionekana wazushi wasiofaa kusikilizwa, bila kujua kwamba mtoto alijificha ndani ya Hoteli ya Lake Tanganyika Beach.

HAKIKA WANAPENDANA: Kama ukaribu wao ulisababishwa na tamasha lililoandaliwa na Zitto peke yake, basi wangekuwa na muonekano ‘feki’ sehemu chache wanazopita lakini kinyume chake wao walithibitisha wanapendana haswaa! Diamond, alishindwa kujichanganya na wasanii wenzake aliokuwa nao kwenye shoo ya Kigoma kama akina Said Juma ‘Chegge’, Peter Msechu, Banana Zorro, Mwasiti Almasi na wengineo, badala yake muda mwingi aliutumia kuwa umbali wa mita sifuri kutoka alipo Wema. Mtundu’ wa nyimbo mbili mpaka sasa, Nai Nai na Baadaye, Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, ndiye pekee aliyekuwa jirani na vijana hao maarufu, walioamua kurejesha penzi lao kupitia mwavuli wa shoo hiyo.

Kwa upande mwingine, ni kama vile waliamua kwenda kufanya tambiko nyumbani asili kwa mume mtarajiwa, yaani Diamond kwa sababu chimbuko la Wema ni Mkoa wa Tabora, japo baba yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu, amejichimbia Zanzibar kwa miaka mingi. Mtu mmoja, mwenye hulka ya kutopitwa na mambo, akamueleza ripota wetu kuwa Julai 18, wasanii hao walikwenda Hifadhi za Gombe na Mahale, mkoani humo lakini jioni yake, Diamond aliongozana na Wema mpaka kwa babu yake, eneo la Ujiji Posta, mkoani humo ambako walisomewa dua na Babu Nasibu.

22 July 2012


Picha kwa hisani ya Salma Msangi Kimora

20 July 2012


Assalaamu ‘Alaykum wa RahmatuLlaah wa Barakaatuh

Tunawatakia Ramadhani Njema Wasomaji wote 
wa 
Tmark-Turn

Insha'Allah Mwenyezi Mungu 
Atutakabalie sisi na nyinyi matendo yetu.

"Taqabbala Allaahu Minna wa Minkum" 

13 July 2012

 My gals
 Maishallah
 Mwari wangu umependeza maishallah mwaaaah




 Kibakuli cha mix sio hahahahah





 Maishallah na mkweo mwenyewe miaka 1000



 Mie hinna tu


 Tenaaa lzm tu......

 Maishallah






 Tanga Oyeeeeeh




2 July 2012


.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!