24 September 2012



 Kampuni ya kusafirisha mizigo ya Serengeti freight Forwarders LTD ya nchini   Uingereza leo imekabidhi misaada kutoka kwa watanzania waishio nchini humo kwa ajili ya kuwachangia wahanga wa mafuriko yaliyotokea mwezi desemba 2011 Jijini dar es salaam. 
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mecky Sadiq akipokea misaada toka kwa mwakilishi wa Serengeti bwana Chris Lukosi,kwa niaba ya wananchi wa Mabwepande.


Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa mabwepande mkuu wa mkoa wa dar es salaam Meck sadiq amewataka watanzania wengine waliopo nje ya nchi kutoa misadaa wakati inapohitajika.

Akikabidhi misaada hiyo muakilishi wa Kampuni ya Serengeti bwana Chris Lukosi alisema kwa kuwathamini wananchi hao waliothirika na mafuriko,kampuni yake iliamua kuisafirisha mizigo bure kama mchango wao kwa wahanga. 

Awali akikabidhi misaada hiyo muakilishi wa kampuni ya serengeti,amewashukuru,mmiliki wa blog ya Miss jestina george na Urban Pulse kwa kuweza kushirikiana nao katika kukamilisha zoezi zima la ukusanyaji wa misaada hiyo.

Viongozi wa kampuni ya usafirishaji wa mizigo ya serengeti bwana Chris Lukosi wakiwa na mkuu wa mkoa wa Dar esa salaam Said Mecky Sadiq(wa pili kulia)mara baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Uingereza. 

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!