16 May 2012  • KATIKA kuonyesha kuwa fani ya Urembo inazidi kuchukua kasi nchini Tanzania,lukaza blog imeamua kujikita kudhamini shindano la redds miss higher learning Dodoma 2012.
    Shindano la Redds Miss higher learning Dodoma linatarajia kufanyika siku ya ijumaa  wiki hii katika ukumbi wa Kilimani uliopo mjini humo.
    Akizungumza na timu ya Tmark-turn blog,mmiliki wa blog ya Lukaza ,Bwana Joseph Lukaza alisema ameamua kudhamini shindano hilo ili kuweza kuongeza tija kwa washiriki na kuondoa fikra potofu zinazojengwa na Jamii kuwa fani ya urembo ni ya kihuni.
    Viingilio katika shindano  hilo 15,000 kwa upande wa VIP na 10,000 kwa mzunguko wa kawaida,mzee wa magubegube atakuwepo katika kuusindikiza usiku huo.
Reactions:
Categories:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!