28 April 2012



Rotavirus ni nini?

Huu ni ugonjwa wa kuhara unaoshambulia watoto wa chini ya miaka mitano. Inasemekana karibu watoto wote lazima waupitie ugonjwa huu wakiwa wameafikia umri huu wa miaka mitano hadi kumi.

Dalili kuu

Mtoto huanza kutapika akifuatiwa na kuharisha sana, pamoja na homa. Hivi vinasababisha mtoto aishiwe maji mwilini, kitu ambacho kinasababisha vifo vingi vinavyohusiana na ugonjwa huo.

Kimbilia hospitali ukiona…

Kuharisha zaidi ya mara nne ndani ya muda wa masaa 12.
Kutapika
Homa
Kama mzazi, hakikisha unakwenda upesi hospital usidharau, hutopoteza kitu (hasahasa pesa kidogo) ukienda daktari akakwambia hamna kitu.pata picha utakavyojilaumu kwa kuchelewa kwenda hospital

Unaambukizwaje?

Kama ilivyo kwa magonjwa mengi ya matumbo hasa ya kuhara, ugonjwa huu huambukizwa kupitia kula vitu vichafu vinavyoingizwa mdomoni hivyo wazazi wenye watoto wanaotambaa muwe makani na watoto hili msisite kuwaelewesha na wadada wanaobaki na watoto.
Pia ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kwa kupitia mfumo wa hewa.


Kinga

Huu ugonjwa una chanjo, ila hii ni kwa wale walio nchi zilizoendelea aka nchi za mbele, hapa kwetu hamna kitu kama hicho. Kwa kuwa unaambukizwa mara nyingi kwa uchafu, tujitahidi kuhakikisha watoto hawaweki vitu vichafu mdomoni, wananawa mikono kabla ya kula na baada ya kwenda maliwatoni, kina dada nao wafanye hivyo hivyo,na kuhakisha unanawa baada ya kumbadilisha mtoto nepi,diapers ama pampers


Tiba

Mara nyingi madaktari watampa dawa za kutibu hao virusi na matibabu ya kawaida ya mgonjwa wa kuhara.

TAHADHARI:
Usikimbilie kununua dawa kabla hujamwona daktari, dawa za bakteria hazitibu virusi.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!