21 June 2014

Uvitaji wa Shisha ni sawa na uvutaji wa sigara kulingana na madaktari

Waziri wa afya nchini Tanzania, amesema kuwa Tanzania inapanga kutathmini sheria ya sasa kuhusu matumizi ya Sisha ili kufanya mageuzi au kubadili sheria hiyo matumizi ya Shisha.

Dkt Seif Rashid Selemani amesema kuwa sheria hiyo italenga kulinda afya ya watanzania hasa walio na uraibu wa Shisha na pia kuhakikisha kuwa wanaotumia Shisha katika sehemu zengine duniani wanapata kubadili mfumo wa maisha ili kulinda afya zao.

Uraibu huo unaohusisha uvutaji wa Tumbaku yenye ladha tofauti tofauti ambayo hutiwa ndani ya chupa kubwa na kuvutwa kwa mirija, umeshika kasi sana Tanzania hasa miongoni mwa vijana mjini Dar Es Salaam.Hii ni baada ya taarifa ya awali kuwa serikali ilikuwa tayari imechukua hatua kupiga marufu bidhaa hiyo ambayo inaenziwa sana hasa na vijana.

Baadhi ya watu wanaiona Shisha kama isiyokuwa na madhara ya kiafya ikilinganishwa na uvutaji wa Sigara.

Lakini wataalamu wanaamini kuwa uvutaji wa Shisha kwa muda wa saa moja ni sawa na kuvuta sigara miamoja.

Madaktari walitoa onyo kuhusu uvutaji wa Shisha wakisema kuwa waraibu wanakabiliwa na tisho la kuugua Saratani sawa na hatari inayowakabili wavutaji wa sigara.

Habari kwa hisani ya BBC SWAHILI 

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!