Wanawake wazee nchini Kenya, wamehamua kujifunza Karate kwa nia ya kujilinda na uzalilishaji unaowatokea mara kwa mara na haswa matukio ya kuwabaka na unyanyasaji mwngine.
Mmoja wa wazee hao ni bibi Wairimu Gachenga, mwenye umri wa miaka 70,
ambaye anaishi katika makazi duni (slum) ya Korogocho jijini Nairobi.
Akiwa na majukumu ya kuwatunza na kuwalea wajukuu zake wawili Wahome
Njeri (19) na Wairimu Njeri (7). Amekuwa na majukumu hayo baada ya mama
yao kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Wanawake hao wazee, wamehamua kufanya mazoezi ya kujilinda baada ya mmoja wao kubakwa. Kesi za kuwabaka vizee nchini Kenya ziekuwa zikiripotiwa mara kwa mara, lakini juhudi za polisi za kuwafikisha waharifu hao mikononi mwa sheria zimekuwa ndogo sana, kiasi cha wazee hawa wa kike kuamua kujikusanya pamoja na kujifunza namna ya kujilinda na kuchunga usalama wa kila mmoja wao.
0 comments:
Post a Comment