Skendo iliyokuwa ikiendelea mtaani kuhusu msanii Diamond na tuhuma za kumrekodi aliyekuwa mpenzi wake wa zamani mwanadada Wema Sepetu, msanii huyo amekir kuwa ni kweli alifanya tuhuma hizo kwaajili ya kulinda penzi lake.
“Hivi karibuni Wema amekuwa akinipakazia mbovu kwa mpenzi wangu Penny akiwa na lengo la kutaka kuni haribia juu ya mimi na mpenzi wangu, nilichukia sana kwahiyo siku alivyoamua kunipigia simu ndipo niliamua kumrekodi ili kumsikilizisha Penny ambaye alikuwa haniamoni kabisa” Alifunguka Diamond.
Sauti hiyo ambayo ilitoka kwa Wema Sepetu ikiwa inambembeleza Diamond waweze kurudiana pamoja kwakuwa bado anampenda, Diamond amekiri kuirekodi hiyo sauti lakini amekana kuisambaza mitaani na hajui nani kafanya hivyo.
“Lengo langu kubwa ilikuwa ni kurekodi sauti hiyo na kumsikilizisha Penny, sasa ambaye aliichukua na kuisambaza mitaani sijui ni nani, lakini hata mi sikujisikia vizuri nilipoisikia mitaani maana sikupenda hali iwe hivyo lakini ndo sina jinsi” aliongeza Diamond.
Baada ya kukiri kujutia, Diamond aliambiwa aombe msamaha Live ili Wema asikie ila alikataa na kusema hawezi kumuomba msamaha maana haoni kosa lake.
Vijimambo blog

0 comments:
Post a Comment