7 June 2012


Mwanafunzi wa darasa la kwanza Obeid Manase mwenye umri wa miaka 8 Manase mkazi wa kijiji cha Kigadye wilayani Kasulu mkoani Kigoma amefariki dunia baada ya bomu kulimlipukia mikononi alipokuwa akicheza na wenzake.

Bomu hilo lilimlipukia mtoto huyo wakati alipokuwa akitupiana wenzake wakati walipokuwa wakicheza.

Kamanda wa polisi mkoani Kigoma kamishina msaidizi wa polisi Frasser Kashai alisema tukio hilo limetokea Juni sita mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni katika kijiji cha Kigadye kata ya Herushingo tarafa ya Makere wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Alisema watoto watano walikuwa wakilichezea bomu hilo na kuwalipukia na kusababisha kifo cha mmoja wao ambaye alifariki papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa.

Amewataja watoto waliojeruhiwa katika tuko hilo kuwa ni Tuju Seluke(7), mwanafunzi wa darasa la kwanza aliyejeruhiwa tumboni, Angel Seluke (4) ambaye alijeruhiwa sikio la kushoto, Sarah Manase(6) aliyejeruhiwa paja la kulia na Isaack Yohana(4) aliyejeruhiwa jicho la kushoto ambao wote wamelazwa katika hospitali ya Heri Mission wilayani Kasulu na hali zao zinaendelea vizuri.

Akizungumzia bomu hilo lililosababisha kifo cha mtoto huyo kamanda Kashai alisema uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi umebaini kuwa watoto hao walilichukua bomu hilo kwenye maua sehemu inayoaminika kuwa lilifichwa na baba yake mdogo na marehemu aitwaye Ayub James na Juhudi za kumtafuta kwa mahojiano zinaendelea.
Categories:

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!