6 August 2014

Inaelezwa kuwa benki ya mbegu za kiume itatatua haja za uzazi
Benki ya Taifa ya mbegu za kiume inatarajiwa kuanzishwa nchini Uingereza kuondokana na tatizo la upungufu wa mbegu hizo.

Wapenzi wa jinsia ya kiume na kike , wale wa jinsia moja pia wanawake wasio na wenza watanufaika na huduma hii mpya ambapo kutoka jamii zisizofahamika watakuwa na uwezo wa kuchagua wachangiaji kutoka katika jamii nyingine.

Benki hii itakayosimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Gamete na Hospitali ya Wanawake ya Birmingham itafunguliwa mwezi Oktoba.

Mradi huu umetengewa paundi 77,000 na Idara ya Afya nchini Uingereza.
Kituo hiki kitakuwa katika hospitali ya wanawake mjini Birmingham ambacho kitakuwa kikihifadhi mbegu hizo.

Hivi sasa kumekuwa na upungufu wa wachangiaji wa mbegu za kiume nchini Uingereza hasa katika hospitali za taifa,huku kukiwa na ongezeko la uhitaji, hospitali hizo zikitibu tatizo hilo linaloelezwa kuwa kubwa nchini humo.

Mfuko huo umesema una matumaini kuwa uwepo wa benki hiyo utapunguza idadi ya wagonjwa wanaojiweka katika hatari kwa kutafuta huduma hii bila kufuata taratibu.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!