23 July 2013

KUNA WIMBI LA MATAPELI WAPO HASA MAGOMENI MAPIPA NA SASA WANATUMIA AKINA MAMA NA WATOTO WA KIKE KUANZIA MIAKA TISA NA KUENDELEA. WATOTO HAO UNAWAKUTA WAMEBEBA MTOTO ANAKUSALIMIA NA KUKUOMBA MSAADA KWA KIGEZO KUWA ALIKUWA SAFARINI YEYE NA MAMA YAKE WAMEPATA AJALI NA MAMA YAKE AMEFARIKI DUNIA, NA YEYE HANA PA KWENDA KWANI HAJUI KWA NDUGU ANAOMBA MSAADA,HUKU ANALIA NA MTOTO ALIYEBEBWA NAYE ANALIA, UKIWA KAMA MZAZI HURUMA INAKUJIA, UKIENDELEA KUONGEA NAE NI KOSA HAPO NDO ANATOKEA MKAKA AMBAYE ANADAI KUWA AMEMPA LIFT BAADA KUONA ANALIA KWA HIYO ANAOMBA ASAIDIWE ILI APATE PA KWENDA KULALA.
 
HUYO KAKA ANADAI KUWA HAWEZI KUMCHUKUA KWANI NI BINTI MDOGO NA YEYE HANA MKE WATU WATAMWLEWA VIBAYA. HAPO WAMESHAKUTEKA KIMAZINGIRA UANAKUWA HUJITAMBUI TENA KILA WANACHOKUAMBIA UNAKUBALI TU KAMA ZOBA, WANAONDOKA NA WEWE WANACHUKUA KILA KILICHO CHAKO. KISHA WANAKUSHUSHA POPOTE PALE WANATAKA WAO. WANAKUACHA MWEUPEE, BAADAE NDO AKILI INAKUJIA. WAMEPATA MKASA HUU NI WATU WENGI SANA, NAOMBA MLIONGELEE HILI NADHANI WATU WENGI WATATOA USHUUDA KWA NJIA YA SIMU. HATUNA SEHEMU YA KULIONGELEA HATA UKIENDA POLICE UNAJISUMBUA, WATU WENGI SANA NIMESIKIA WAKILALAMIKA KUHUSU HILI.
TUSAIDIE ILI WATU WAWE MAKINI WASISALIMIANE NA MTU AMBAE HAWAMJUI .
 
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!