12 April 2013


NI kivumbi! Kuna madai kwamba, staa wa Bongo asiyechuja, Wema Sepetu amemfikisha mama yake, Miriam Sepetu kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar kwa madai ya kwenda nyumbani kwake na kufanya vurugu zilizosababisha kuharibika kwa samani mbalimbali.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilijiri usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, jijini Dar.
Mbali na mama mtu, wengine waliofikishwa kituoni hapo ni dada mkubwa wa Wema aitwaye Nuru na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Bestizo ambaye inasemekana ni mshirika mkubwa wa Diamond kwenye masuala ya mtandao wa msanii huyo.
“Wema alikuwa nyumbani kwake usiku huo, watuhumiwa hao wakamzukia na kuanza kumchapa makofi ya ‘kelbu’ ambapo katika mshikemshike huo, baadhi ya vitu vilivunjika na kumtia hasara staa huyo,” kilisema chanzo.
Haikujulikana mara moja ni kitu gani kilisababisha mama mzazi huyo, dada mtu na kijana asiyekuwa ndugu kwenda kwa Wema na kutenda kosa hilo.
Wema alikwenda polisi na kuandikisha maelezo ambayo yameingizwa kwenye jalada lenye kumbukumbu; KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MALI.
Chanzo:global publisher

Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!