22 February 2013

Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kanyenye Mkoani Tabora Michael Fidelis ameamua kujinyonga baada ya kutofurahishwa na matokeo yake ya kidato cha nne yaliyotoka mwaka huu.

Mwanafunzi huyo aliamua kujinyonga baada kupigiwa simu na rafiki yake akimtaka akaangalie majibu kwani yameshatoka.

Akizungumza kwa niaba ya familia Kaka wa marehemu alisema“tangu jana saa 11 marehemu alikua hai ila kuna mwanafunzi mwingine yuko Mbeya ambae ni Rafiki yake alimpigia simu na kumueleza majibu yameshatoka hivyo baada ya kukuta majibu sio mazuri ndipo alipoamua kuchukua uamuzi Wa kujiua."Alisema kaka wa marehemu

Alisema marehemu ametumia kamba ya manila katika kufanikisha zoezi lka kujiua,ameendelea kwa kusema  ujumbe aliouacha ulikua unaishilizia ukisema… mama mimi nakupenda, nimejinyonga kwa sababu matokeo ya form four sio mazuri.

Akimzungumzia marehemu rafiki yake wa karibu alisema kuwa yeye na marehemu walianza wote kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Kanyenye mpaka walipomaliza kidato cha nne mwaka jana.

Alisema marehemu alikuwa akijitahidi sana katika masomo na pia walikuwa wakihudhuria wote masoma ya ziada(tution)darasani alikuwa mtu mzuri mpole na msikivu,hakuwa mkorofi kwa walimu wala wanafunzi wenzie.

Ameendelea kusema kuwa marehemu alifanya vizuri sana katika mtihani wake wa mock,hivyo alikuwa na uhakika hata matokeo yake ya mtihani wataifa yatakuwa mazuri pia,hivyo hakutegemea kama yatakuwa tofauti kama yalivyotoka.

Michael amejiua katika chumba alichokuwa amepangiwa na familia yake kwa ajili ya kujisomea karibu na nyumbani.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!