28 September 2012  • Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe amesema hatogombea tena nafasi ya ubunge 2015 katika jimbo lake.
    Amesema atafanya kampeni ya Urais, kama mgombea wa CHADEMA au kama mpiga debe wa mgombea wa CHADEMA. 
    Ameyaandika haya katika ukuraha wake mtandao wa kijamii wa facebook leo,amesema miaka 10 ya Ubunge inamtosha na kwa ngazi hiyo ni vema awaachie wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa kigoma. 
    Amesema huo ndio uamuzi wake wa mwisho na ameshawaeleza wananchi wa Jimbo lake la mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005.
    tmark-turn inakutakia kila la kheri katika uamuzi wako bwana Zitto Kabwe,ni matumaini yetu viongozi wengine wataiga mfano wako.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!