24 September 2012
Wakati mwingine inabidi tuishi kiubishi maana ukifatilia nani atasema nini kuhusu wewe ndugu mafanikio utayaona kwa wale wanaoshi kwa kuangalia mioyo yao inasema nini.
Sio kila anaekuchekea anamaanisha amekufurahia na sio kila anaekununia anakuonea wivu pengine anawaza ni jinsi gani na yeye atafikia mafanikio uliyonayo au hata zaidi yake na pia kuna wengine wako tu ili mradi wanaishi ukifanya zuri kwao baya naukifanya baya ndo umeharibu kabisa,kwako wewe unayenitangazia kuwa  nimezaa bila ya kuolewa Kweli wewe uko  kwenye kundi la wale ambao wapo tu ilimradi wanaishi pole sana na ninakuhakikishia sitopoteza muda wangu kukuwekea picha zangu za harusi ili kukuthibitia mwezi gani niliolewa na mwezi gani nilijifungua binti yangu.Na ninakuhakikishia sijakuchukia wewe na yoyote yule mwenye kunisema vibaya hapa duniani.
Na kwanini sijakuchukukia ni kwasababau ninawapenda sana watu wote ambao wananichukia na ninajua mpo wengi sana.
Ila  kwa wewe ningekushauri tu kabla hujazungumza kitu kuhusu mtu fulani akikisha unachotaka kukisema kama kina ukweli ndani yake.
Usiwe unajiropokea tu.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!