4 June 2012

                                                                 Musa Mateja na Shakoor Jongo
WEMA Isaac Sepetu ‘Pedeshee Mwanamke’, amefanya kufuru mpya baada ya kuvuta mkoko wa maana wenye thamani ya Sh. milioni 38 na kumpa mama yake, Miriam Sepetu ule usafiri aliokuwa akitumia wa Toyota Lexus Harrier.
Wema ambaye ni tishio katika filamu za Kibongo na umodo alifanya tukio hilo Mei 25, mwaka huu kwa kile alichodai kuwa aliona mama yake anateseka na usafiri kwani siku chache gari la mzazi wake huyo alilokuwa akitumia lilipata hitilafu.
AINA YA GARI
“Ni Toyota Mark X. Muda mrefu nilipanga kununua gari la kifahari lakini kitendo cha kuharibika kwa gari la mama kimechochea mimi kununua gari hili,” alisema Wema.
ANAPATA WAPI JEURI?
Ni kitambo sasa, Wema kama ilivyo kwa Jacqueline Wolper, amekuwa hana shida ndogondogo kwa kuwa mkwanja anao wa kutosha na kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu, amenunua gari hilo ili kuwathibitishia kuwa fedha siyo tatizo kwake kwani ana ‘mnene’ anayemuwezesha.
Habari kwa Hisani ya: www.globalpublishers.info
Reactions:
Categories:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!