1 November 2013

 Serikali ya Tanzania imetangaza kufuta daraja sifuri katika matokeo ya elimu ya sekondari nchini na kuongeza daraja la tano ambapo pia matokeo ya kidato cha nne kwa watahiniwa wanaorudia mitihani yatahusisha matokeo yao ya awali wakati wakiwa shuleni ili kuwarahisishia kupata alama nzuri.

Katibu mkuu wa Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi Profesa Sifuni Mchome amesema pamoja na marekebisho hayo pia wameongeza daraja B ya juu kwa alama za ufaulu ambapo daraja A wigo wa ufaulu ni kati ya alama 75 na 100, daraja B la juu ni kati ya alama 60 na 74, daraja B la kati ni 50 na 59, daraja C kati ya 40 na 49, daraja D kati ya 30 na 39, daraja E kati ya 20 na 29 na daraja F ni kati ya alama 0 na 19.

Profesa Mchome amesema marekebisho hayo yanalenga kuinua kiwango na kuboresha kiwango cha elimu Tanzania ambapo kwa kila muhitimu wa kidato cha nne matokeo yake ya mwisho yatajumlishwa na alama zisizozidi 40 ambazo zitatokana na majibu ya mitihani ya kidato cha pili, cha tatu na mtihani wa Mock.

Kwenye sentensi nyingine ni kwamba mtihani wa kidato cha nne utafanyika November 4 2013 ambapo zaidi ya Watahiniwa laki nne wanatarajiwa kufanya mtihani hii ambapo kati yao, Watahiniwa laki 3 na elfu 67,399 ni kutoka shuleni huku Wavulana ni 198,257 sawa na asilimia 53.69 na Wasichana ni 169,142 sawa na asilimia 46.04 ambapo vituo vya kufanya mitihani ni 4,365


Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!